Notification texts go here Contact Us Buy Now!
TENGENEZA BLOG YA BIASHARA KUPITIA WAT_TECHNOLOGY...
Posts

MAGEMU MAZURI YA KUCHEZA KWENYE SIMU (ANDROID)

 


Kama wewe ni mpenda magemu na unatumia simu yako ya Android kucheza magemu basi hapa tumekuandalia orodha ya magemu machache ambayo unaweza ya cheza na ukafurahia zaidi muda wako wa kucheza magemu kwenye simu yako. Kama ndio kwa Mara ya kwanza unataka kujifunza au kuanza kucheza magemu ya Android basi ni vema ukaangalia magemu yalio katika orodha hii na ukaangalia linalo kufaa kisha ukalipakua.


Call of Duty mobile



Hili ni gemu zuri sana la kivita ambalo limetolewa na Activision. Gemu la Call of Duty mobile ni gemu lililochezwa na watu Wengi na Mpaka sasa linaendelea kuchezwa na mamilioni ya watu ulimwenguni. Kama unapenda magemu ya kivita basi gemu hili unaweza kulifulahia zaidi lakini unachotakiwa kujua nikwamba game hili ni la Online. Kwa lugha nyingine tunaweza kusema gemu hili linahitaji internet ili kulicheza. Kitu kizuri kuhusu magemu hili ni kwamba unaweza kucheza na watu wengine na pia Kuna mode ningine za kucheza zinazoweza kufanya usichoke kulicheza. Ili kulipata kirahisi gusaHAPA


Bus Simulator Indonesia




Bus Simulator Indonesia ni moja ya magame ambayo huchezwa na watu wengi sana na mpaka sasa limechezwa na watu wasiopungua Milioni 50 na wengi hulifahamu kwa jina lake la BUSSiD. Ni game lililotolewa mwaka 2017. Game hili ni la Online yaani ili kulicheza utahitajika kutumia data. Kama nimpenzi wa game za muundo huu basi hakikisha unapakua game hili maana ni game zuri sana.Kitu unachotakiwa kukifahamu ni kwamba mazingira na magari yalio katika game hili yanayofana na mazingira ya Indonesia ndiomana likawa na jina Indonesia.Linaweza kuchezwa na watu zaidi ya mmoja (Online). Linapatika playstore kwa MB zisizopungua 572. Unaweza kulipakua kirahisi kwa kugusa HAPA


 Traffic Rider



Kama ni mtu unaependa magame mazuri na unavutiwa zaidi na game za pikipiki basi game la Traffic Rider ni game litakalokufurahisha zaidi.
Game hili mpaka Sasa limechezwa na watu zaidi ya Milioni 7 ulimwenguni na asilimia kubwa ya watu hao wamelipenda.
Linamuonekano mzuri, Sauti zenye uhalisia na majira yenye uhalisia maana kuna hadi mission za usiku. Kadr unavyoendesha kasi pikipiki na kuovertake magari ndivyo unavyojiongezea idadi ya Scores. Lina missions zaidi ya 70 na kuna zaidi ya pikipiki 20 tofauti tofauti.Traffic Rider ni game lipatikanalo Playstore na lina MB90 tu. Hukubali mpaka katika simu zenye RAM 1 bila shida yoyote. Kama utahitaji kulipata kirahisi game hili gusa HAPA

Occupation 2.5



Ni gemu ambalo unalicheza ukiwa Kama mtu ambae upo kwenye mji uliochafuka na kila mtu naeishi katika mji huo anaishi kwa hofu kubwa kutokana na uwepo wa wafu wanaotembea yaani Zombies na baadhi ya viumbe vingine visivyo na urafiki na binadamu. Ni moja ya magame mazuri yanayopatikana kwa Mbs chache katika playstore. Lina nyumba zinaingilika na unawachezesha wahusika zaidi ya mmoja katika mji huo. Unaweza kulipata kirahisi game hili kwa kugusaHAPA


EA Sports UFC



Unapenda magemu ya kupigana? Kama Unapenda magemu ya kupigana basi gemu la EA Sports UFC ni game ambalo halitakiwi kukoswa kwenye simu yako. Gemu hili ni moja ya magemu mazuri sana ya kupigana. Lina muonekano mzuri mno ambao utakufanya ufurahie kulicheza. Linahusu kupigana kwa kutumia ngumi na mateke.
Limekusanya wapiganaji wengi maalufu duniani ambao utatakiwa kuwafungua kutokana na uchezaji wako. Gemu hili linaweza kuchezwa Offline na Online. Ukiwa unacheza Online unakua na uwezo wa kucheza na watu wengine toka sehemu mbalimbali za dunia na utatakiwa kupambana nao na kufanya wapoteze dira kwa vitasa(ngumi) na mateke ya mitindo mbalimbali ili uibuke mshindi. Unaweza lipata katika playstore kwa kugusa HAPA

Overkill 3




Hili ni gemu zuri sana la Action ambalo mpaka sasa limechezwa na watu zaidi ya milioni 5. Linamuonekano mzuri na watu wengi wanalipenda kutokana na muonekano wake unaofanana na Caver Fire. Gemu hili huchezwa bila data (Offline) pia linaweza kuchezwa na watu zaidi ya mmoja kwa kutumia data (Online).Inashauriwa anaecheza gemu hili awe na miaka 16 na kuendelea. 
Overkill 3 ni gemu lipatikanalo Playstore kwa kama MB 401 ivi na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa HAPA



Takashi Ninja Worriror: Shadow of last samurai





Hili ni moja ya magemu mazuri sana ambayo kwa sasa yako trend katika playstore. Gemu hili ni la kijapani na linamuhusu kijana Takashi ambae anaingia katika kulipa kisasi kutokana na watu wake kufanywa vibaya. Ukilipakua utaweza kulicheza muda wowote na bila kukugharimu chochote maana gemu hili huchezwa bila data (Offline) pia hupatikana kwa MB chache sana zisizopungua MB 100.
Unaweza kulipata kirahisi katika playstore kwa kugusa HAPA


Modern Strike Online






Ni moja ya magemu bora ya kivita ambayo huchezwa Online tu. Limechezwa na watu wengi sana wasio pungua Milioni hamsini(50).Gemu hili ni moja ya magemu yanayofanana na gemu la Call of duty hivyo kama unapenda magemu ya jamii ya Call of duty, usiache kucheza game hili.
Katika game hili unaweza cheza na marafiki zako Online kwa kiunda timu ya kuwaangamiza maadui au mukashindana kuua maandui ili atakaewaua maadui wengi awemshindi.
Modern Strike Online ni gemu lipatikanalo Playstore kwa MB zisizopungua gb 2.2. Unaweza lipata kirahisi kwa kugusa HAPA




Real Moto




Kama ni wewe ni mpenzi gemu za mashindano ya pikipiki basi real moto linaweza kuwa bora sana kwako. Game hili huchezwa bila kutumia data yaani ni gemu la Offline. Limechezwa na zaidi ya watu Milioni kumi(10). Utaweza kutunza kumbukumbu zote za gemu hilo kwenye email yako ili simu ikipotea uendelee kucheza palepale ulipoishia kucheza gemu hilo pindi utakapopata simu nyingine na kuiingiza email yako.
Gemu hili hupatikana playstore kwa MB 170. Unaweza kulipata kirahisi sana kwa kugusaHAPA



Garena Free Fire





Garena Free Fire linatumia data na lipo hivi; Unamchagua mtu wako utakaemchezesha kisha unatupwa katika eneo moja na wenzako 49 wanaocheza gemu hilo muda huo duniani ili mupigane na uwemzima. Kwaiyo kila mtu utakaemuona katika gemu hili ni mtu anaepambania maisha na anaecheza kama wewe.
Zaidi ya watu Milioni 500 ulimwenguni wanalicheza Gemu hili kupitia vifaa vyao vya Android. Ni gemu linalopendwa na watu wengi kutokana na kuwa dogo kuliko magemu mengine ya muundo huu ambayo ni PUBG na CODM. 
Unaweza kulipakua katika playstore kwa MB 674 pia unaweza rahisisha upatikanaji wake kwa kugusa HAPA



Rarry Fury: Extrime racing



Kama unapenda gemu za magari usiache kupakua gemu hili lenye utofauti mkubwa na magemu ya magari yanayotamba kila mwaka. Game hili ni moja kati ya magame yanayopendwa na watu na mpaka Sasa limepakuliwa na zaidi ya watu Milioni 50. Linauhalisia wa kufurahisha wa mashindano ya Rarry.
Ukiachilia mbali muonekano wa game hili kuwa mzuri pia game hili linawezwa chezwa na mtu mmoja Offline au zaidi ya moja Online.Lina chukua kama MB 150 kulipakua na linapatikana katika playstore. Unaweza lipata kirahisi kwa kugusa HAPA




eFootball 



Ukiongelea gemu kali za mpira wa miguu katika mwaka huu huwezi acha game hili. Gemu hili limepakuliwa na watu wengi sana hapa duniani na hii ni kwasababu liko vizuri. Kama umeshawahi cheza magemu ya PES basi tambua kuwa “eFootball” ni lile lile PES ila wamebadilisha jina tu.

Linachezwa Online na inashauriwa kuwa na mtandao usiosumbua ili uweze kulifaidi gemu hili bila usumbufu.Hupatikana playstore kwa GB 2.0 pia unaweza kulipata kirahisi sana kwa kugusaHAPA



Real Boxing


Hili ni gemu la mchezo wa ngumi ambalo mpaka sasa limechezwa na watu wasiopungua Milioni 10 ulimwenguni. Lipo vizuri sana kwanzia muonekano hadi sauti za vitasa(Ngumi). Kama ni mpenzi wa magemu ya kupigana, usikubali kuliacha gemu hili maana ni gemu lenye uhalisia wa mchezo wa kupigana wa Boxing.
Inashauriwa anaecheza game hili asiwe na miaka chini ya kumi na sita (16+). Game la Real Boxing hupatikana playstore kwa kama MB 321 ivi na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusaHAPA






Dream league Soccer ⚽️ 



(DLS) ni gemu lingine la mpira au soka linaliweza kucheza kwenye simu simu. Gemu hili lilitolewa na First Touch games limited. Katika gemu hili unaweza kuunda timu yako ya ndoto na kusaini wachezaji wako unaowakubali wa mpira wa miguu kwenye timu yako.
Internet huitajika ili kucheza gemu hili kwa sababu ni DSL ni gemu linalihitaji data kulicheza. Lakini kulipakua na kuicheza ni bure ingawa ukihitaji, unaweza kununua baadhi ya vitu ndani ya gemu kwa pesa halisi.
Kulipata hili game kwa urahisi gusaHAPA



PIA UNAWEZA KUPATA MAGAME HAYA YAKIWA HACKED UNLIMITED MONEY 💰 COIN 🪙 GOLD, DIAMOND 💎  ETC

KWA MSAADA ZAIDI BONYEZA HAPA


Post a Comment

Whatsapp me 0699181313
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.